20 Oktoba 2025 - 18:51
“Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimewapiga maadui zao Kofi lisilosahaulika”

Jenerali Mousavi alisema kuwa kipindi cha masomo ya kijeshi kwa wanafunzi hao kilitokea katika wakati wa kipekee - wakati ambao muqawama ulithibitisha ushindi wa imani juu ya dhulma na ubabe wa kimataifa.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Meja Jenerali Seyyed Abdolrahim Mousavi, Mkuu wa Majeshi ya Iran, amesema kuwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimewapa maadui wao kisasi kikali kisichosahaulika, licha ya mipango ya muda mrefu ya adui iliyoandaliwa kwa miaka 15.

Akizungumza katika sherehe ya mahafali ya wanafunzi wa Chuo cha Kijeshi cha Imam Ali (a.s) na vyuo vingine vya maafisa wa kijeshi vilivyoshiriki kwa njia ya mtandao, Jenerali Mousavi aliwapongeza wahitimu na kuwaita “maafisa wa mstari wa mbele wa muqawama (upinzani)” na “viongozi wa baadaye wa jeshi la Iran.”

Maelezo ya Hotuba

Jenerali Mousavi alisema kuwa kipindi cha masomo ya kijeshi kwa wanafunzi hao kilitokea katika wakati wa kipekee - wakati ambao muqawama ulithibitisha ushindi wa imani juu ya dhulma na ubabe wa kimataifa.

Ameongeza kuwa: “Leo dunia inaiheshimu Iran kwa imani, ujasiri, mshikamano na azma yake. Ulimwengu umeamini nguvu ya muqawama. Palestina imekuwa jina pendwa duniani na Gaza imegeuka kuwa kielelezo cha uthabiti na ushindi wa damu juu ya upanga.”

Matokeo ya Operesheni “Tofaan al-Aqsa”

Amesema kuwa operesheni Tufan al-Aqsa imekuwa mwanzo wa matukio makubwa katika eneo na duniani.

“Wamarekani na Wazayuni ambao kwa miaka mingi walijionesha kama wenye haki kupitia mitandao yao ya propaganda, sasa wamefichuliwa kama wauaji wa watoto na wanyama wa damu. Sauti ya haki na mateso ya Wapalestina sasa inasikika duniani kote.”


Kuhusu Msukumo wa Iran na Kushindwa kwa Adui

Mousavi alieleza kuwa mtazamo wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran umejidhihirisha kuwa wa haki na wa kimisingi: “Iran inapolinda wanyonge na waliodhulumiwa, inasimama upande sahihi wa historia. Na inapokataa ubabe, hilo ni dalili ya busara, heshima na uhuru.”

Amesema kuwa Israel kwa msaada wa Marekani ilijaribu kuishambulia Iran ili kujiokoa kutokana na fedheha, hasira ya ulimwengu na mgawanyiko wa ndani — lakini ilishindwa vibaya na kulazimika kuomba kusitishwa kwa vita.

Vita vya Kisaikolojia na Vyombo vya Habari

Mousavi ameeleza kuwa maadui sasa wanajaribu kuficha kushindwa kwao kupitia vita vya habari na akili (cognitive war): “Tunapambana na vita vya kubadilisha fikra na imani za watu. Kile ambacho hawakuweza kukipata kwa silaha, sasa wanajaribu kukipata kwa propaganda, uongo na operesheni za kisaikolojia.”

Amewataka wanajeshi, vyombo vya habari, wasomi na taasisi za kielimu kuongeza uelewa, kuzalisha fikra na kutoa tafsiri sahihi za ukweli, kwani vita vya leo ni vita vya maana na simulizi (narrative warfare).


Tahadhari na Uwezo wa Kijeshi 

“Sisi si wenye kutaka vita, lakini tuko tayari. Tunafahamu kanuni za kusitisha mapigano, lakini endapo watathubutu tena, hatua zetu zitakuwa tofauti kabisa,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Ayatollah Sayyid Ali Khamenei), kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa hekima ya wananchi wa Iran, maadui walipigwa vibaya na kupata fundisho lisilosahaulika.

Wito kwa Wanafunzi wa Kijeshi

Mousavi aliwahimiza wahitimu wa kijeshi kuwa na:

a) Maadili ya juu na kujenga nafsi (maendeleo ya kiroho);

b) Ujuzi wa kisasa wa kijeshi na teknolojia;

c) Mazoezi ya mwili na uimara wa kisaikolojia;

d) Ubunifu na uvumbuzi katika vita vya kesho;

e) Uelewa wa undani wa vita vya akili na namna ya kupambana navyo.

Hitimisho

Akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwepo kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, alisema:

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mara elfu kwa neema ya kuwepo kwa Kiongozi wetu Mtukufu. Tunaomba kivuli chake kitue juu ya wote wanaotafuta haki duniani.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha